WIKI YA SHERIA MKOANI KATAVI KUADHIMISHWA
Wananchi wilaya ya mpanda mkoani katavi wametakiwa kujenga tabia ya kutembelea sehemu zinazotoa haki ili kupata uelewa wa masuala mbalimbali yanayohusu mahakama.
Rai
hiyo imetolewa na hakimu mkazi mfawidhi Omar Hassan wakati akizungumza na
mpanda redio ambapo ameeleza kuwepo mazoea kwa wananchi kuhitaji
msaada mahakamani pindi wanapokuwa na matatizo ya kisheria.
Aidha amebainisha njia ambazo
mahakama imekuwa ikitumia katika utoaji elimu na msaada wa kisheria kwa
wananchi ikiwemo mabango na kuwaalika wananchi kuhudhuria kusikiliza kesi
mbalimbali zinazoendeshwa katika mahakama ya wazi.
Katika hatua nyingine amesema maadhimisho ya wiki ya sheria mkoani katavi yanatarajiwa kufanyika katika viwanja vya mahaka ya manspaa ya mpanda kuanzia tarehe 27 hadi 31 na kilele kufanyika tarehe mosi February huku kauli mbiu ikiwa ni “matumizi ya Tehama katika utoaji haki kwa wakati na kuzingatia maadili”.
Kila
mwaka mahaka ya Tanzania huadhimisha siku ya sheria ambayo huashiria kuanza
rasmi kwa shughuli za mahakama kwa mwaka.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments