MAAMUZI YA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA ZANZIBAR
KAMATI ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa
Kaskazini Pemba Omar Khamis Othman imelazimika kutengua makubaliano ya zamani
ya uchukuaji wa mizigo katika bandari ya Wete. Kamati hiyo imesema imetengua
makubaliano hayo baada ya kubaini kuwepo na mgogoro kati ya vikundi
vya uchukuzi bandarini hapo.
Vikundi vya uchukuzi ambavyo vilikuwa katika
mgogoro wa uchukuzi wa mizigo bandarini hapo ni Shikamana na
Dausheni ambapo makubaliano hayo yalikuwa ni kwa wanachama wa Shikamana kubeba
mizigo kwenye meli wakati Dausheni kubeba mizigo inayoingia bandarini hapo kwa
njia ya majahazi .
Baada
ya kufuta maamuzi hayo,Serikali imeutaka uongozi wa Shirika la bandari Tawi la
Pemba kusimamia mgawanyo sawa wa uchukuzi wa mizigo wa meli na
majahazi.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments