WANANCHI WATAKA ELIMU YA USALAMA BARABARANI MPANDA
Wananchi katika halmashauri ya Manispaa Mpanda mkoa katavi wamelitaka jeshi la polisi kutoa elimu juu ya alama za barabarani ili kupunguza ajali .
Wakizungumza kwa nyakati tofauti watumiaji wa barabara
wamesema elimu ya usalama barabarani itawasaidia watembea kwa miguu kujiepusha
na ajali za mara kwa mara zinazotokea kwa kutokujua matumizi ya alama hizo.
Kamanda wa usalama barabarani mkoa Katavi John Mfinanga
amesema elimu ya usalama barabarani na matumizi ya alama wanazitoa kupitia
radio na katika vijiwe vya bodaboda ili kuwasaidia watembea kwa miguu kuweza
kuzifahamu sheria na alama hizo.
Mfinanga ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi
pindi semina hizona kusema kwamba semina hizo zinatolewa bure na hazina malipo.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments