MKURUGENZI MKOANI KATAVI ATAKA TV IKANUSHE HABARI ZA UONGO ILIZOTANGAZA KUHUSU HALMASHAURI YAKE
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi Michael Nzyungu,amekanusha taarifa zilizotangazwa na kituo cha Televisheni cha Azam ambacho kimeripoti kuwa Halmashauri haijafikia malengo ya makusanyo ya mapato kwa mwaka wa fedha 2017/2018.
Bw.Nzyungu
ametoa ufafanuzi huo wakati akizungumza na Vyombo vya habari Ofisini kwake.
Aidha Bw.Nzyungu
pamoja na mambo mengine amevishauri vyombo vya habari kutumia waandishi wenye
umahiri wa kuandika habari ili kufikisha taarifa sahihi kwa jamii.
Kwa mjibu wa
MkurugenziTaarifa hizo zilichukuliwa kupitia kikao cha baraza maalumu la
madiwani lililokuwa likijadili rasmu ya bajeti ya mwaka wa fedha 2018/2019.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments