AMEHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA JELA KWA KOSA LA KUBAKA MTOTO
Mahakama ya wilaya ya Mpanda
mkoani Katavi imemuhukumu Willson John(34)
mkazi wa Kijiji cha Simbwesa wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi
kutumikia jela kifungo cha maisha baada ya
kupatikana na hatia ya kumbaka mtoto (7)wakati akiwa anaoga
bafuni.
Hukumu hiyo ilitolewa jana na hakimu mkazi
mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Mpanda Chiganga Tengwa baada
ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande
wa mashtaka.
Kabla ya kusoma hukumu hiyo hakimu Tengwa alisema mtu
yoyote anaefanya kitendo kama alichofanya
mshitakiwa huyo anakuwa amefanya kosa kinyume cha
kifungu cha sheria namba 130 kifungu kidogo cha kwanza na 2E
cha sheria namba 131
kidogo cha tatu cha kanuni
ya adhabu.
Alieleza kutokana na ushahidi
uliotolewa mahakamani na upande wa
mashtaka uliotolewa na mashahidi sita akiwemo mtoto
aliyebakwa ambapo
mshitakiwa hakuwa na shahidi yoyote na
mahakama imeridhika na ushahidi huo wa upande
wa mashtaka.
Hakimu Tengwa alisema miongoni mwa ushahidi
uliomtia mshitakiwa hatiani ni ule uliotolewa na
mtoto mwenyewe aliyefanyiwa kitendo hicho pia daktari aliyemfanyia
uchunguzi na kuthibitishwa kuingiliwa kwa mtoto huyo
kwenye sehemu zake za siri na kuharibiwa
hali iliyomlazimu kumwanzishia dawa za kumkinga na maambuzi
ya VVU.
Pia ushahidi mwingine ni wa mama mzazi wa
mtoto huyo ambaye aliutoa mahakamani kuwa mtoto wake alibakwa.
Awali katika kesi hiyo mwanasheria wa Serikali Fravian
Shiyo alidai mahakamani hapo kuwa mshitakiwa John alitenda
kosa hilo Septemba 24 mwaka huu majira ya saa 2:30 usiku
nyumbani kwao na mtoto huyo
ambako mshitakiwa alikuwa
amepanga chumba kwenye nyumba yao wazazi
wa mtoto aliyembaka na wakati antenda kosa hilo wazazi wa mtoto huyo walikuwa
wakiangalia mpira sebuleni kwenye TV.
Alieleza siku ya tukio hilo
mtoto huyo alikua amechukua maji kwaajiri ya
kuingia bafuni kuoga wakati
alipokaribia kwenye mlango wa bafuni
alimkuta mshitakiwa akiwa
amesimama karibu na mlango wa
kuingilia bafuni na ndipo
mshitakiwa alipomtolea kauli na kusema wewe ingia
tuu bafuni uoge
na mie nakuja kupata
haja ndogo humo humo.
Mwanasheria shiyo
alisema wakati mtoto huyo akiwa
anaendelea kuoga mshitakiwa Willson aliingia
ndani ya bafu na kumziba mdomo iliasipige kelele
mtoto huyo na kisha na kisha alianza kumbaka
na alipomaliza alimwachia mtoto huyo
na kumwambia kuwa endapo angemwambia
mtu yeyote juu ya kitendo alichomfanyia
atamuua.
Aliendelea kuieleza mahakama hiyo aliyebakwa
awe mwoga na asiwaambie
wazazi wake na aliingia ndani na kumwomba
Mama yake ampatie maji ya kunawa
hata hivyo mama yake alimkatalia
kumpa maji kwa kile alichodai mbona ametoka kuoga muda si mrefu
maji ya nini tena.
Ndipo mtoto huyo
alipoingia ndani ya
chumba alichokuwa akilala hata hivyo
alishindwa kupata usingizi kutokana na maumivu
yalivyozidi alimwagiza mtoto mwezake
wa kike amwite mama yake na
alipoingia chumbani
alimkuta akiwa analilia huku godoro alilokua amelalialikiwa limelowa damu na ndipo alipomtaja mtuhumiwa
kuwa ndio aliyembaka.
Kabla ya kusomewa hukumu mshitakiwa
alipewa ya nafasi
ya kujitetea kama anayosababu ya msingi
ya kuishawishi mahakama imwone hana
hatia au impunguzie adhabu.
Katika utetezi wake mtuhumiwa alidai kuwa
yeye hakutenda kosa hilo
isipokuwa ni chuki za mama
wa mtoto huyo ambaye alikuwa amemwongezea
kodi ya chumba kutoka shilingi 20,000 hadi 40,000 ambazo yeye mshitakiwa
alikataa kulipa ongezeko hilo.
Utetezi huo ulipingwa vikali na mwendesha mashitaka
wakili wa Serikali ambae aliiomba
Mahakama itowe adhabu kali kwa mshitakiwa ili iwe fundisho kwenye jamii kwa watu wenye tabia kama hiyo
.
Hakimu Ntengwa baada ya
kusikiliza utetezi huo na pingamizi la
upande mashitaka alisoma hukumu
na kusema kuwa mtuhumiwa
amahukumiwa kutumikia jela kifungo
cha maisha yake yoye na kama
hajaridhika na uamuzi huo anayo nafasi ya kukata
rufaa kwenye mahakama ya juu
ya ngazi nyingine na kisha alimpatia nakala ya
hukumu hiyo na kwenda nayo gerezani.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments