RAIS MAGUFULI AMETOA MSAADA MSIKITINI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe
Magufuli ametoa msaada kwa Msikiti wa Noor Mkange, Miono, wilayani ya Chalinze
mkoa Mkoa wa Pwani leo.
Waumini wa dini ya Kiislam wa Msikiti wa Noor uliopo
katika Kijiji cha Mkange,Miono,Wilaya ya Chalinze Mkoa wa Pwani,wamemshukuru
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe Magufuli kwa msaada wa
zulia la kuswalia na fedha taslim Shilingi milioni Mbili.
Zulia
pamoja na fedha hizo zimekabidhiwa na Msaidizi wa Rais Kanali Mbaraka Mkeremy
kwa niaba ya Rais Dkt.John Pombe Magufuli kwa Imamu wa Msikiti huo Alhaji
Sheikh Khamis Nassor wa Msikiti Noor uliopo katika kijiji cha Mkange, Wilayani
Chalinze mkoa wa Pwani.
Kanal
Mkeremy kwa niaba ya Rais Magufuli, amewataka waumini wa Msikiti huo kutumia
msaada huo kwa lengo lililokusudiwa.
Sheikh
Nassor mara baada ya kukabidhiwa Msaada huo amesema,kwa niaba ya waumini wa
Msikiti huo wamemshukuru Mhe.Rais kwa kuitikia ombi lao la kupata zulia na
kwamba kwa kutimiza ahadi yake hiyo Mhe.Rais amedhihirisha kuwa yeye ni mtu wa
watu asiyebagua dini wala kabila katika kusaidia jamii ya kitanzania.
Aidha
Sheikh Nassor amesema waumini wa msikiti huo wanamuombea na wataendelea
kumuombea Mheshimiwa Rais na kuwataka watanzania wote nchinikuungana nao
kumuombea Rais bila kujali itikadi za kisiasa ama imani za kidini kwani
anayoyafanya Rais kwa wananchi wa Tanzania ni kwa manufaa ya wananchi wote.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments