JELA MIAKA 30 MKOANI RUKWA KWA KOSA LA KUBAKA MTOTO
MAHAKAMA ya wilaya Nkasi mkoani Rukwa imemhukumu kutumikia
kifungo cha miaka 30 Jela,kulwa Dase (35) mkazi wa kijiji cha Paramawe
wilayani Nkasi kwa kosa la kumbaka mtoto wa miaka 15.
Akisoma hukumu hiyo hakimu mkazi wa mahakama hiyo Ramadhan Rugemalila
alisema mahakama imeridhishwa pasipo kuacha shaka yoyote na ushahidi uliotolewa
na upande wa mashtaka na hivyo kumuhukumu mtuhumiwa kifungo hicho.
Alisema kufuatana na mwenendo wa kesi hiyo ambapo mashahidi
wanne walitoa ushahidi upande wa mashitaka mtuhumiwa alikutwa na
hatia chini ya kifungu cha sheria f namba 130(1) na namba (2)(e) NA 131 sura ya
16 ya kanuni ya adhabu.
Awali upande wa mashitaka ukiongozwa na mwendesha mashitaka wa
jeshi la Polisi Hamimu Gwelo uliieleza mahakama hiyo kuwa mtuhumiwa alitenda
kosa hilo Agosti 12 mwaka huu majira ya saa 8 mchana.
Aliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa mtuhumiwa ili iwe
fundisho kwa watu wengine baada ya vitendo kama hivyo kukithiri katika
siku za hivi karibuni.
Mahakama hiyo ilipompa nafasi ya kujitetea mtuhumiwa aliomba
mahakama isimpe adhabu kali kwa maana hilo ni kosa la kwanza kwake na anategewa
na familia yake.
Baada ya utetezi huo mahakama iliamua kutoa hukumu ya kwenda
jela miaka 30.
Hukumu hiyo ilitolewa juzi.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments