WANAFUNZI SHULE YA BIBLIA FPCT KATUMBA WAMETEMBELEA KITUO CHA MPANDA RADIO,MENEJA WA KITUO ATOA NENO KWAO
Na.Issack Gerald
Wanafunzi 17
walimu 3 wa shule ya biblia FPCT Katumba Wilayani Mpanda Mkoani
Katavi,wametembelea kituo cha Mpanda Radio na kueleza kuridhishwa na namna kinavyosaidia jamii katika masuala mbalimbali
ya kijamii.
Mara baada ya
kutembelea kituo hiki,Mkuu wa shule ya biblia FPCT Mchungaji Elisha Musenda
pamoja na kuipongeza Mpanda Radio kwa
namna inavyohudumia wananchi amesema kuna kila sababu ya kituo hicho kufika
mbali zaidi kimatangazo.
Kwa upande wake
Meneja wa kituo cha Mpanda Radio Bw.Levokatus Msafiri,amesema kituo kitaendelea
kushirikiana na kila mwananchi kwa lengo la kuchochea maendeleo bila kujali
itikadi ya mtu.
Aidha
Meneja Msafiri ametoa wito kwa wanafunzi hao ambao pia ni viongozi wa
dini katika maeneo wanayotka kutumia nafasi yao waliyonayo kuelimisha jamii
namna ya kuondokana na tatizo la mimba za utoto,Kutumia vyandarua kujikinga na
mbua waenezao maralia pamoja na
mapambano dhidi ya maambukizi ya Ugonjwa hatari wa Ukimwi kutokana na Mkoa wa
Katavi kuwa mkoa wenye hali ya kiwango cha juu katika matatizo hayo.
Kwa upande wake Kalenga Jailos ambaye
mwenyekiti wa wanafunzi waliofika katika kituo cha Mpanda Radio akizungumza na kwa
niaba ya wanafunzi wenzake amewashauri watnazania kutumia Mpnda Radio kwa kuwa
ipo kwa ajili ya kuwahudumia .
Mpaka sasa
Mpanda Radio imetimiza miaka minne tangu ianze kurusha matangazo yake mwaka
2013.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments