RAIS WA LIBERIA ATIMULIWA
Rais anayemaliza muda wake nchini Liberia,Ellen Johnson Sirleaf,ametimuliwa
katika chama chake kwa tuhuma za kutomuunga mkono mgombea wake ili amrithi.
Chama
chake cha Unity kinamtuhumu Bi.Ellen, kwa kuwahamasisha wananchi kutompigia
kura mgombea ambaye alikuwa Makamu wa Rais Joseph Boakai.
Aidha,chama
hicho kinamtuhumu kwa kukiuka Katiba kwa madai ya kumfanyia kampeni George
Weah,ambaye aligombea kupitia chama cha Coalition for Democratic Change na kuibuka
mshindi.
Bw.Weah
ambaye ni mwanasoka nyota wa zamani, anatarajiwa kuapishwa rasmi Januari 22 mwaka
huu ikiwa ni mara ya kwanza Liberia kushuhudia mabadiliko ya uongozi kwa njia
ya amani tangu mwaka 1944.
Chanzo:EATV
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments