MELI YA MAFUTA ILIYOKUWA IKITEKETEA MOTO IMEZAMA BAHARINI
Meli ya mafuta ambayo imekuwa
ikiteketea kusini mwa bahari ya China kwa zaidi ya wiki moja hatimaye imezana
REUTERS
Meli ya mafuta iliyokuwa ikiteketea moto imezama baharini.
Kwa mjibu wa vyombo vya habari vya
China,Sanchi na meli nyingine ya mizigo ziligongana kilomita 260 nje ya
Shanghai Januari 6 mwaka huu ambapo baadaye ilianza kusombwa kusini mashariki
kwenda Japan.
Maafisa wa Iran sasa wanasema
Meli hiyo ilikuwa imebeba tani 136,000 za mafuta lakini maafisa wanasema kuwa hakuna hatari kubwa. wahudumu
wote 32, wakiwemo raia 30 wa Iran na wawili raia wa Bangladesh wote walifariki.
Meli hiyo ilikuwa imebeba tani
136,000 za mafuta lakini maafisa wanasema kuwa hakuna hatari kubwa ambapo Meli
zingine 13 na kikosi kutoka Iran wamekuwa wakishiriki katika jitihada za kuokoa
licha ya kuwepo hali mbaya ya hewa.
Siku ya Jumamosi wafanyakazi walikuwa
wameingia kwenye meli hiyo ambapo walipata miili ya wahudumu wawili ndani ya
mashua ya kuokoa maisha huku Waokoaji walipata kisanduku cha kurekodi sarafi
lakini wakaondoka haraka kutokana kuwepo moshi na joto jingi.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments