MBUNGE CHADEMA MKOANI KATAVI AIBUKA NA HOJA YA KUPATIKANA DIWANI MWINGINE WA KATUMBA
Mbunge
wa viti maalumu mkoa wa Katavi kupitia
Chadema Rhoda Kunchela amesema kitendo cha kata ya Katumba halmashauri ya Nsimbo
mkoani Katavi kutokuwa na diwani ni kuchelewesha maendeleo kwa wananchi wa kata
hiyo.
Hayo
yamebainishwa leo na Mbunge huyo na kusema kuwa wananchi wanakosa
uwakilishi na kushauri uchaguzi ufanyike
ili apatakane diwani mwingine.
Katika
hatua nyingine Mh Kunchela amezungumzia
ziara aliyoifanya mwenyekiti wa Bawacha taifa
Halima Mdee amabye pia ni mbunge wa jimbo la kawe na kusema ziara hiyo imefanyika mkoani katavi ikilenga
kuimarisha uhai wa chama hicho.
Diwani
aliyekuwa akiongoza kata hiyo Mh Seneta Baraka mwezi Novemba mwaka jana alihukumiwa
kifungo cha miaka mitatu jela kwa kosa la kupokea rushwa.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments