BARAZA LA MAASKOFU KUTEMA CHECHE KESHO KUHUSU HALI YA USALAMA WA TANZANIA NA WATU WAKE
Baraza la maaskofu wa kanisa la
Kiinjili la Kilutheri chini Tanzania (KKKT) linasema umoja na amani ya Tanzania
viko hatarini.
Katika waraka wa ujumbe wa pasaka
unaosambaa katika mitandao ya kijamii na kutarajiwa kusomwa kesho katika
makanisa mbali mbali ya KKKT nchini Tanzania, baraza hilo limeorodhesha mambo
kadhaa ambayo wameyataja kuwa ndio tishio la umoja na amani ya nchi hiyo.
Waraka umeyataja baadhi ya mambo hayo
kuwa ni pamoja na utekaji,utesaji,kupotea kwa watu, mashambulizi ya silaha
dhidi ya viongozi wa kisiasa,mauaji yenye mwelekeo wa kiitikadi,vitisho,
ubambikiziaji wa kesi na matumizi mabaya ya vyombo vya dola dhidi ya wananchi.
Waraka umeongeza pia kwamba uhuru wa
kujieleza,kutoa na kupokea habari umeendelea kutoweka nchini huku ukionya
kubanwa na hatimaye kuelekea kupungua kwa uhuru wa Bunge,Mahakama, na Tume ya Uchaguzi,
ukisema hatua hii ni pamoja na kudhoofishwa kwa serikali za Mitaa.
jumbe huu kutoka baraza la maaskofu
wa KKKT umekuja siku chache tu baada ya ujumbe wa Kwaresima uliotolewa na
baraza la Maaskofu wa kanisa Katoliki
Maaskofu wa Katoliki waligusia pia
kuminywa kwa uhuru wa kutoa na kupokea habari huku wakitaja baadhi ya vyombo
vya habari kufungiwa au kusimamishwa kwa muda.
Walionya kwamba katika mazingira haya
ni rahisi kwa jamii kufarakana na hata kujenga chuki kiasi cha kuhatarisha
amani, usalama na hadhi ya uhai wa binadamu.
Maaskofu wa KKKT wameasa kwamba roho
iliyokuwemo kwa waasisi wa taifa na hata kusaidia kupata uhuru mwaka 1961 bila
kumwaga damu,inapaswa kuendelea wakati wote.
Habari zaidi ni WWW.P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments