RAIS MAGUFULI ATEUA WAKURUGENZI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Dkt.John Magufuli amefanya uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki(TAEC),Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC),Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa na Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Benjamini Mkapa Dodoma.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema Rais Magufuli amemteua Prof.Lazaro Busagala kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki kuanzia tarehe 22 Machi mwaka huu ambapo kabla ya uteuzi huo Prof.Busagala alikuwa Makamu Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) – Taaluma na Utafiti.
Aidha ameteuliwa Prof.Damian Gabagambi kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) kuanzia machi 22 mwaka huu ambapo  anachukua nafasi ya Bw.Mlingi Elisha Mkucha ambaye atapangiwa kazi nyingine.
Kabla ya uteuzi huo Prof.Gabagambi alikuwa Mhadhiri wa Uchumi wa Chuo Kikuu cha Kilimo – Sokoine (SUA).
Wengine ni Dkt.Deodatus Michael Mutasiwa ambaye ameteuliwa kuwa  Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma,Dkt. Alphone Bilola Chandika kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma ambapo kabla ya Uteuzi huu Dkt.Chandika alikuwa akikaimu nafasi hiyo.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA