ZANZIBAR YAPAA MAAMBUZI YA KIFUA KIKUU
Wizara ya Afya Zanzibar imesema kasi
ya Ugonjwa wa kifua kikuu imekuwa ikiengezeka kwa kiwango kikubwa ambapo katika mwaka 2017 jumla ya wagonjwa 948 waligundulika
kuwa na ugonjwa huo.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari
kuhusiana na siku ya kifua kikuu katika ukumbi Wizara hiyo Mnazi mmoja Mjini
Zanzibar ,Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Muhammed amesema Ongezeko hilo
limefikia idadi ya wagonjwa 225 ikilinganishwa na mwaka 2016.
Amesema kutokana na ongezeko hilo
Utafiti unaonesha bado Zanzibar inakabiliwa na tatizo la Uelewa mdogo juu ya
Maradhi hayo jambo ambalo linapelekea wananchi kushindwa kuhudhuria katika
vituo kwa wakati ili kupunguza maambukizi.
Amesema kutokana na Ugonjwa wa kifua kikuu kuwa ni
ugonjwa wa tisa unaosababisha vifo kwa wagonjwa serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar itahakikisha inachukuwa jitihada mbalimbali ikiwemo kuendelea kutoa elimu ya kujiepusha na
viashiria vya maradhi hayo.
Kwa mujibu wa ripoti ya shirika la
Afya ulimwenguni takwimu zinaonesha kuwa kwa Tanzania ni nchi ya 30 ulimwenguni
zenye idadi kubwa ya wagonjwa wa kifua kikuu ambapo kwa mwaka 2016 jumla ya
watu milllioni 10.4 wameugua ugonjwa huo kati yao wagonjwa Millioni 1.6
walifariki dunia.
Aidha Waziri Hamadi ametowa wito kwa
Viongozi wa serikali ,Wadini na Siasa kutumia nafasi walizonazo katika taasisi
zao na Mkutano kutoa elimu juu ya Ugonjwa wa maradhi ya kifuua kikuu ili
kupunguza tatizo la uhaba wa elimu katika jamii.
Kwa upande wake Mkuu wa kitengo
shirikishi cha Homa ya Inni,kifua na Ukoma
Farhat Khalid amesema ni vyema kwa wananchi kuachana na visababishi vya
Maradhi ya kifua kikuu ikiwemo Ulevi na uvutaji sigara ili kutokomeza ugonjwa
huo Nchini.
Aidha ametowa wito kwa jamii kufika
katika vituo vya afya baada ya kujigundua kuwa wanadalili za Ugonjwa huo ili
waweze kunufaika na huduma za matibabu kwa wakati.
Siku ya kifua kikuu huadhimisha kila
ifikapo March24 ambapo kwa mwaka huu siku hiyo inatarajiwa kuadhimishwa katika
ukumbi wa baraza la wawakilishi la Zamani Mjini Unguja ikiwa na ujumbe Usemao ‘’TUNAHITAJI VIONGOZI MAHIRI WA KUONGOZA
MAPAMBANO YA KUMALIZA KIFUA KIKUU’’.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments