TANZANIA YASHTUSHWA KUHUSISHWA NA KOREA KASKAZINI-Septemba 16,2017
Tanzania imesema imeshtushwa baada ya kuorodheshwa miongoni mwa nchi
ambazo zimechunguzwa na Umoja wa Mataifa na kuhusishwa kuwa na uhusiano wa
kibiashara na Korea Kaskazini.
Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam,waziri wa mambo ya nje Dkt.Augustine Mahiga,amesema
licha ya uhusiano uliokuwepo awali, lakini tangu mwaka 2014,Tanzania imepunguza
kabisa uhusiano wa kibiashara na kidiplomasia na nchi hiyo.
Aidha Waziri Mahiga amesema
uhusiano huo wa kibiashara ulikuwepo kabla ya vikwazo vilivyowekwa hivi
karibuni na Baraza la Umoja wa Mataifa.
Waziri huyo amesema anaelekea katika
mkutano wa kawaida wa Umoja wa Mataifa, ambapo atatumia fursa hiyo kujibu
tuhuma hizo kwa Baraza la Usalama.
Tanzania na Uganda ni
miongoni mwa baadhi ya nchi zinazochunguzwa na Umoja wa Matiafa kwa tuhuma za
kwenda kinyume na vikwazo vilivyowekwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
dhidi ya Korea Kaskazini.
Ripoti ya uchunguzi huo
ilitolewa mnamo tarehe 9 mwezi wa Septemba. Baraza la Usalama la Umoja wa
Mataifa limesema linachunguza tuhuma za Tanzania kuingia mikataba ya kijeshi na
Korea Kaskazini inayogharimu dola za kimarekani milioni 12.5.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments