UNDENI VIKUNDI FEDHA KWA AJILI YA WATU WENYE ULEAMAVU ZIPO-Septemba 16,2017
SIKU moja
baada ya Shirikisho la watu wenye Ulemavu Shivyawata Mkoani Katavi kuomba watu
wenye ulemavu kuwezeshwa ili kujikwamua kimaisha na hatimaye kujenga uchumi wa
taifa,halmashauri ya Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi imewataka watu wenye
ulemavu kuunda vikundi vya kijasiliamali ili wapatiwe mikopo.
Kauli hiyo
imetolewa leo na Mkurugenzi Mtendaji Manispaa ya Mpanda Bw.Michael Nzyungu
kuhusu haki ya watu wenye ulemavu katika kupatiwa mikopo ili kufanya shughuli
za maendeleo.
Bw.Nzyungu
amesema fedha ipo isipokuwa wanachosubiri ni vikundi vya watu wenye ulemavu
kujitokeza ili kupatiwa mikopo hiyo yenye masharti nafuu.
Aidha
amesema mpaka sasa kwa mwaka wa fedha 2016/2017 Manispaa ya Mpanda imetoa
Shilingi milioni thelathin (30,000,000/=) kwa vikundi vya wajasiliamali ambapo
watu wenye ulemavu hawamo katika kiasi hicho kutokana na kutokuwa na vikundi.
Halmashauri
ya Manispaa ya Mpanda katika bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018 imetenga
shilingi bilioni mbili kwa ajili ya asilimia 10 zinazotolewa kwa vikundi vya
wajasiliamali wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.
Katika
mgawanyo wa asilimia 10 kwa makundi hayo ambapo ni sawa na shilingi milioni
200,wanawake hupata asilimia 4 vijana asailimia 4 huku watu wenye ulemavu
wakipata asilimia 2 ambapo kwa kiasi
kikubwa wanawake wameonekana kujitokeza kupata mikopo hiyo kwa wingi
ukilinganisha na vijana wanaojitokeza kwa uchahche huku kukiwa hakuna watu
wenye uleamavu wanaojitokeza.
Siku ya
jana Shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu Shivyawata Mkoani Katavi
kupitia kwa mwenyekiti wa shirikisho hilo Bw.Issack Lucas Mlela liliomba
serikali iwapatie mikopo watu wenye ulemavu ili kujikwamua kimaisha.
Makundi ya watu wenye ulemavu mkoani
Katavi yanahusisha walemavu wasioona,walemavu wa viungo,viziwi,walemavu wa
akili,walemavu wenye tatizo la usonji na wenye ulemavu wa ngozi Albino ambapo
jumla ya watu wenye ulemavu mkoani Katavi wanakadiriwa kuwa zaidi ya 1000
wakiwemo wanafunzi karibu 100 wanaosoma katika shule za msingi Kashato,Nyerere
na Azimio zenye vitengo maalumu kwa ajili ya watoto wenye ulemavu.
Kwa mjibu wa sheria namba 9 ya mwaka
2010 iliyopitishwa na bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania mwaka 2010 ,serikali
pamoja na jamii kwa ujumla inawajibika kuhakikisha watu wenye ulemavu wanapata
haki sawa na wale wasio na ulemavu katika sekta mbalimbali ikiwemo Elimu, Afya,
Uchumi, Biashara na huduma nyingine muhimu kwa ajili ya binadamu.
0764491096
Comments