SHIVYAWATA WAOMBA WATU WENYE ULEMAVU WAWEZESHWE ILI KUJIKWAMUA KIUCHUMI-Septemba 15,2017
SHIRIKISHO la vyama vya watu wenye
ulemavu Shivyawata Mkoani Katavi,limesema watu wenye ulemavu mkoani Katavi bado
wanahitaji kuwezeshwa zaidi kama makundi mengine yasiyo na ulemavu ili
kujikwamua kimaisha na kujenga uchumi wa taifa.
Mwenyekiti wa shirikisho hilo Mkoani
Katavi Bw.Issack Lucas Mlela amesema,makundi ya watu wenye ulemavu yameendelea
kuishi katika maisha magumu kutokana na kutopewa kipaumbele kama sheria ya nchi
inavyoelekeza.
Aidha Bw.Mlela ameyapongeza mashiriki
binafsi ambayo yamekuwa yakitoa semina kwa watu wenye ulemavu ili kutambua haki
yao na wajibu wa jamii kuhusu makundi hayo.
Makundi ya watu wenye ulemavu mkoani
Katavi yanahusisha walemavu wasioona,walemavu wa viungo,viziwi,walemavu wa
akili,walemavu wenye tatizo la usonji na wenye ulemavu wa ngozi Albino ambapo
jumla ya watu wenye ulemavu mkoani Katavi wanakadiriwa kuwa zaidi ya 1000
wakiwemo wanafunzi karibu 100 wanaosoma katika shule za msingi Kashato,Nyerere na
Azimio zenye vitengo maalumu kwa ajili ya watoto wenye ulemavu.
Kwa mjibu wa sheria namba 9 ya mwaka
2010 iliyopitishwa na bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania mwaka 2010 ,serikali
pamoja na jamii kwa ujumla inawajibika kuhakikisha watu wenye ulemavu wanapata
haki sawa na wale wasio na ulemavu katika sekta mbalimbali ikiwemo Elimu, Afya,
Uchumi, Biashara na huduma nyingine muhimu kwa ajili ya binadamu.
0764491096
Comments