NDOA ZA JINSIA MOJA ZAMFIKISHA MAHAKAMANI-Septemba 16,2017
Kijana mmoja aliyetambulika kwa jina la
Sharifu Issah maarufu kama Zamda Salumu Mkazi wa Manispaa ya Mtwara,
amefikishwa mahakamani kwa kosa la kufanya vitendo vya utovu wa kimaadili kwa
kujifanya mwanamke na kumshawishi mwanaume mwenzake kufunga ndoa.
Akisoma kesi hiyo
hakimu mkuu mkazi Richard Kabate amesema kosa hilo ni kinyume na kifungu cha
157 cha kanuni ya adhabu sura namba 16 ya sheria iliyofanyiwa marekebisho mwaka
2002.
Kabate
amedai kuwa mshtakiwa kati ya mwezi Machi na mwezi wa Juni mwaka huu akiwa katika
vijiji vya Mkahala na Mpanyani halmashauri ya Nanyamba mkoani Mtwara kwa
makusudi alijifanya mwanamke na kumshawishi Mustapha Saidi Nurdini kwa
kumtongoza na kufunga nae ndoa isiyo halali.
Hata
hivyo hakimu Kabete amesema kitendo hicho kinatoa tafsiri ya ukiukwaji mkubwa
wa maadili kwa watu wa jinsia moja ya kiume kuishi kinyumba.
Mara
baada ya Mshtakiwa kusomewa shtaka hilo
na wakili wa serikali George Makasi amekana shitaka hilo na upelelezi wa kesi
hiyo unaendelea.
Mshtakiwa amerudishwa
mahabusu na kesi hiyo itatajwa mahakamani hapo Septemba 28 mwaka huu ambapo dhamana
iko wazi baada ya mwezi mmoja.
0764491096
Comments