WAPENZI WA JINSIA MOJA WAKAMATWA ZANZIBAR-Septemba 16,2017
Kwa mjibu wa Afisa mkuu wa Polisi
Zanzibar Hassan Ali,Wanawake 12 na wanaume 8 walikamatwa kufuatia uvamizi wa
polisi katika hoteli moja ambapo washukiwa hao walikuwa wakishiriki katika
warsha.
Mapenzi ya jinsia moja ni uhalifu nchini
Tanzania na ngono miongoni mwa wanaume ni hatia inayomtia hatiani mhusika na
kufungwa kifungo cha kati ya miaka thelathini jela na kifungo cha maisha.
Mwezi Septemba mwaka 2016,serikali
ilisitisha kwa muda miradi ya ukimwi ya wapenzi wa jinsia moja ambap pia mwezi
Februari mwaka huu,serikali ilisitisha huduma za vituo 40 vya afya vya
kibinafsi kwa madai ya kutoa huduma kwa wapenzi wa jinsia moja.
Comments