RAIS MAGUFULI AMLILIA MZEE KINGUNGE NGOMBALE MWIRU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli,amepokea kwa huzuni na masikitiko taarifa za kifo cha mmoja wa waasisi wa Taifa na mwanasiasa mkongwe nchini Mzee Kingunge Ngombale Mwiru.
Kifo
cha Mzee Kingunge Ngombale Mwiru kilichotokea usiku wa kuamkia leo majira ya
saa 10:30 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam.
Mzee
Kingunge Ngombale Mwiru alikuwa akipatiwa matibabu hospitalini hapo baada ya
kushambuliwa na mbwa wake nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam 22 Desemba 22
mwaka jana.
Mhe.Rais
Magufuli amesema Taifa limempoteza mtu muhimu ambaye alitoa mchango mkubwa
katika juhudi za kupigania uhuru na baada ya kupata uhuru akiwa mtumishi mtiifu
wa Chama cha TANU na baadaye Chama Cha Mapinduzi (CCM) na katika nyadhifa
mbalimbali za uongozi ndani ya Serikali.
Kwa
mjibu wa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu kufuatia
msiba huu,Mhe.Rais Magufuli amewapa pole wanafamilia wote,wanachama wa
CCM,ndugu,jamaa, marafiki na wote walioguswa na msiba huu,na amewaombea kuwa na
moyo wa subira,uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi hiki cha majonzi.
Mwenyezi
Mungu ailaze roho ya Marehemu Kingunge Ngombale Mwiru mahali pema peponi,Amina.
Habari
zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments