MAREKANI YAPATWA WASIWASI NA KENYA
Marekani imeelezea wasiwasi wake mkubwa juu ya matukio yanayotokea nchini Kenya,ambako kiongozi wa Upinzani Raila Odinga alijiapisha mwenyewe kuwa ''Rais wa Wananchi'' siku ya Jumanne.
EPA
Msemaji
wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani Hearther Nauerth amesema
malalamiko kuhusiana na uchaghuzi nchini Kenya yanapaswa kusuluhishwa kupitia
utaratibu unaofaa wa kisheria.
Ameikosoa
pia serikali kwa uamuzi wake wa kuvifungia vituo vitatu vya serikali,ambavyo
vilijaribu kurusha matangazo ya moja kwa moja tukio hilo la kujiapisha kwa
Raila Odinga.
Chanzo:bbc Swahili
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments