TUNDU LISSU NAYE AMLILIA MZEE KINGUNGE
Mbunge
wa Singida Mashariki (Chadema),Tundu Lissu amezungumzia kifo cha Kingunge
Ngombale Mwiru akisema historia itamkumbuka.
Amesema
Mzee Kingunge alikuwa miongoni mwa wazee wenye historia kubwa na alionyesha
ujasiri mkubwa wa kuhama chama chake cha CCM bila kuhofia kuhudhuriwa kutokana
na mazingira yalivyokuwa.
Kingunge
aliyekuwa kada wa CCM mwenye kadi namba nane,Oktoba 4,2015 alitangaza kukihama
chama hicho na kusema hatojiunga na chama chochote lakini mara kadhaa
alionekana akipanda majukwaa ya upinzani kumnadi aliyekuwa mgombea urais wa
Chadema/Ukawa, Edward Lowassa kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25,2015.
Tundu Lissu ambaye ni Rais wa chama cha wanasheria nchini TLS anapatiwa matibabu nchini ubelgiji baada ya kushambuliwa kwa risasi mwaka uliopita.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments