RAIS MAGUFULI KUWATUNUKU KAMISHENI MAAFISA WAPYA WA JWTZ
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli kesho anatarajia kuwatunuku kamisheni maafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Kwa
mjibu wa taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya
Rais Ikulu Gerson Msigwa kamisheni hizo atazitunuku katika viwanja
vya Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Watakaotunukiwa
kamisheni ni maafisa wapya wa Tanzania na kutoka nchi marafiki waliopata
mafunzo katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli Mkoani Arusha.
Tukio
hilo linatarajia kurushwa moja kwa moja na vyombo vya habari hapa nchini
kuanzia saa 3:00 asubuhi.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments