LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA MZUNGUKO WA PILI KUANZA KESHO
Ligi kuu soka Tanzania Bara inatarajia kuendelea tena hapo kesho kwa mzunguko wa pili kupigwa katika viwanja mbali mbali.
Singida United inayoshika nafasi ya nne katika msimamo wa
ligi ikiwa na alama 27 nyuma ya mabingwa watetezi Yanga SC wenye pointi 28
inajipanga kuingia katika mzunguko wa pili hapo kesho siku ya Jumamosi kwa
kuivaa Mwadui FC majira ya saa nane mchana katika uwanja wa Namfua.
Michezo mingine itakayo pigwa hapo kesho ni Azam FC waliyo
nafasi ya pili kwa kujikusanyia alama 30 katika duru la kwanza itakuwa nyumbani
dhidi ya Ndanda FC mechi itakayopigwa Azam Complex Chamazi jijini Dar es
salaam.
Lipuli FC ya Iringa itakuwa na kibarua kizito nyumbani kwake
itakapocheza dhidi ya Yanga SC iliyo maliza mzunguko wa kwanza kwa kuwa na
pointi 28 ikiwa nafasi ya tatu mtanange utakaopigwa dimba la Samora, wakati
Stand United ikiivaa Mtibwa Sugar uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga.
Tanzania Prisons iliyo na alama 21 ikiwa nafasi ya 6 katika
msimamo wa ligi wata wakaribisha Njombe Mji katika uwanja wa Sokoine Mbeya huku
mchezo wa mwisho siku ya hapo kesho ni Majimaji FC itakapocheza na Mbeya City
uwanja wa Majimaji Ruvuma.
Habari
zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments