MWANASIASA MKONGWE KINGUNGE AFARIKI DUNIA



Mwanasiasa mkongwe hapa nchini Tanzania Mzee Kingunge Ngombale Mwiru(87) amefariki dunia leo alfajiri Ijumaa wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam.
Mzee Kingunge Ngombale Mwiru

Kwa mjibu wa taarifa ambayo imetolewa na mtoto wa marehemu Kinje Kingunge,amesema baba yake amefariki usiku wa kuamkia leo majira ya saa tisa.

Kwa mjibu wa taarifa zilizokuwa zimetolewa mwezi uliopita Mzee Kingunge alikuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kushambuliwa na mbwa nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam mwezi mmoja uliopita.
Rais Magufuli alimjulia hali Mzee Kingunge alipolazwa hospitalini
Mke wa Kingunge Peras Ngombale mwiru alifariki dunia mwanzoni mwa mwezi Januari kutokana na ugonjwa wa kupooza kipindi ambacho Mzee Kingunge alikuwa tayari anapatiwa matibabu ya majeraha hayo.
Mzee Kingunge alikuwa kiongozi mwandamizi nchini Tanzania katika serikali za awamu nne zilizopita na amewahi kushika nyadhifa mbalimbali katika serikali  zikiwemo ukuu wa mikoa ya Tanga na Singida,Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi na Waziri katika wizara mbalimbali.
Kingunge aliyekuwa amehduumu kupitia CCM tangu kuanzishwa kwa chama hicho mwaka 1977 alitembelewa Rais wa Tanzania Dkt.John Magufuli katika Wodi ya Mwaisela iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kumjulia hali mwezi uliopita.
 Kingunge Ngombale Mwiru alizaliwa Mei 30, 1930
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA