RAIS KUZINDUA UKUTA WA MIGODI YA TANZANITE
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.John Magufuli kesho Aprili 6,2018 anatarajia
kuzindua ukuta wa machimbo ya madini wa Mirerani mkoani Manyara.
Hayo
yamesemwa leo na Msemaji Mkuu wa jeshi hilo,Kanali Ramadhan Dogoli wakati
akizungumza na waandishi wa habari makao makuu Upanga-Dar es Salaam.
Kanali
Dogoli amesema shughuli itaanza saa moja na wananchi wanakaribishwa kushuhudia
uzinduzi huo.
Mwishoni
mwa mwezi Septemba mwaka 2017Rais wa Tanzania John Magufuli aliliagiza Jeshi la Ulinzi la Wananchi
Tanzania (JWTZ) kujenga ukuta wa kuzunguka vitalu vya kuanzia A hadi D vyenye
madini ya Tanzanite katika eneo la Mererani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara
ili kudhibiti uchimbaji na biashara ya madini hayo.
Rais
Magufuli alitoa agizo hilo kwenye sherehe ya ufunguzi wa barabara ya Kia -
Mererani iliyofanyika katika eneo la Mererani.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments