MUIGIZAJI MAARUFU NCHINI INDIA,SALMAN KHAN AHUKUMIWA JELA MIAKA MITANO
Muigizaji mkongwe nchini
India, Salman Khan amehukumiwa kwenda jela miaka mitano baada ya kukutwa
na hatia ya kuua wanyama jamii ya swala miaka 20 iliyopita.
Leo Aprili 05,2018 Mahakama Kuu mjini Jodhpur katika jimbo la
Rajasthan nchini India imetoa hukumu hiyo baada ya kumkuta na hatia, huku
waigizaji wenzake Saif Ali Khan, Tabu, Sonali Bendre na Neelam Kothari
wakiachiwa huru baada ya kukutwa hawana hatia.
Salman Khan (52) alishtakiwa kwa kosa la ujangili kwa kuua
wanyama hao (BlackBuck Antelopes) ambao ni wachache nchini India mnamo mwaka
1998.
Kwa mujibu wa mtandao wa Daily Mail,
Salman Khan alifanya tukio hilo katika kijiji cha Kankani wakati aki-shoot filamu
yake ya Hum Saath Saath Hain akiwa na wasanii wenzake watano ambao
wameachiwa leo.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments