MKUU WA MKOA ASIKITISHWA WATOTO KUTORIPOTI SEKONDARI
Mkuu wa mkoa wa Katavi Meja Jenerali
Mstaafu Raphael Muhuga amesikitishwa na wazazi ambao hawajawapeleka shuleni
watoto wao kujiunga na masomo ya sekondari kidato cha kwanza mwaka 2018 baada
ya kufaulu mtihani wa darasa la saba mwaka 2017.
Mkuu wa Mkoa ambaye alikuwa mgeni rasmi ametoa masikitiko yake wakati akifungua vikao vya wadau wa elimu Mkoani Katavi vikao ambavyo vinalenga kujadili,kutathimini na kuchukua hatua dhidi ya vikwazo vinavyosababisha Mkoa wa Katavi kufanya vibaya katika ufaulu wa wanafunzi kwa mwaka 2017 ukishuka kutoka nafasi 3 za juu kitaifa na kufikia nafasi ya 9.
Aidha Muhuga amesema mpaka kufikia
mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu,wanafunzi wapatao 240 wilayani Tanganyika
walikuwa hawajaripoti shuleni ambapo amewataka madiwani wawahamasishe katika
kata zao wawapeleke shuleni watoto wao hata kama hana sare na utaratibu
mwingine utaendelea baadaye kubainisha chanzo cha kukosa sare.
Aidha Mkuu wa Mkoa katika kupunguza
changamoto ya uhaba wa miundombinu ya shule ya Mtakumbuka amechangia shilingi
500,000 kwa ajili ya kusaidia kutatua changamoto ya miundombinu ya shule ya
msingi Mtakumbuka.
Kwa mjibu wa mwenyekiti wa kamati ya shule ya Msingi
Mtakumbuka Bw.Augustino Paul Filimbi amesema shule hiyo yenye matundu 6 ya vyoo matatu yakiwa ya wavaulana
na mengine ya wasichana haina choo cha walimu huku vyumba vinne vya madara
vilivyopo kati ya hivyo viwili kodondoka wakati wowote.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji
Manispaa ya Mpanda Bw.Michael Francis Nzyungu kupitia kikao hicho amesema
wanaendelea kutumia fedha za wahisani mbalimbali wakiwemo P4R,Equip Tanzania na
mapato ya ndani ya halmashauri hiyo ili kutatua changamoto ya miundombinu
katika shule za Manispaa.
Vikao vya wadau wa elimu ambavyo
vimezinduliwa jana katika Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda na vinatarajia
kufikia kilele chake Aprili 16 mwaka huu katika kijiji cha Majimoto Halmashauri
ya Mpimbwe wilayani Mlele ambapo leo vikao hivyo vimeendelea katika Halmashauri
ya Nsimbo.
Hata hivyo takwimu zilizotolewa mwishoni mwa mwaka 2017 na Afisa elimu Mkoa wa Katavi Ernest Hinju zinaonesha
wanafunzi zaidi ya 9000 mkoani Katavi wamekosa kujiunga na kidato cha kwanza
kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa shuleni.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments