BUNDI GANI AMEENDELEA KUTANDA KUHUSIANA NA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA TAIFA STARS?TUMEPOROMOKA TENA VIWANGO VYA FIFA MPAKA NAFASI YA 147 KUTOKA 142
Taifa Stars |
Tanzania imezidi kudidimia katika
viwango vya soka duniani baada ya kushuka kwa nafasi 5 zaidi kwenye viwango vya
Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kwa mwezi Novemba.
Kupitia taarifa iliyotolewa ljana
na Shirikisho la soka duniani FIFA inaonyesha Tanzania inashika nafasi ya
147 kutoka 142 mwezi Oktoba ikiwa imeporomoka kwa nafasi tano kutoka juu.
Kwa
Uganda wa Afrika Mashariki na Kati,Uganda imeendelea kuongoza ikiwa inashika
nafasi ya 75 duniani huku Senegal ikiwa inaongoza kwa Afrika nzima ikiwa
inashika nafasi ya 23 kwenye viwango hivyo vya FIFA.
Kwa
upande wa 10 bora,Ujerumani imeendelea kuongoza ikifuatiwa na Brazil,Ureno,Argentina,Ubelgiji,Hispania,Poland,
Uswisi,Ufaransa na Chile.
Tanzania
ilifanya vibaya kwenye michuano ya CECAFA nchini Kenya mapema mwezi huu pia kwa
mwezi Novemba ilipata sare ya 1-1 dhidi ya Benin.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments