RAIS MAGUFULI APOKEA NA KUZINDUA MAGARI 181 YA MSD,MIKOA MIPYA YATAJWA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mh.John Magufuli amesema serikali inaendelea kupanga mikakati yake kuhakikisha inakarabati na
kujenga vituo na Hospitali zinazotoa huduma za afya nchini ikiwemo mikoa mipya
ya Katavi,Songwe,Geita,Simiyu na Njombe.
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo
katika hafla fupi ya ugawaji wa magari 181 ya Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kwa
ajili ya kusambaza dawa maeneo mbalimbali nchini,uzinduzi ambao umefanyika eneo
la Keko jijini Dar es Salaam.
Aidha Rais Magufuli mbali na
kuwashukuru Global Fund kwa msaada wa magari 181 yasiyokuwa na masharti amesema yatarahisisha huduma
mbalimbali katika maeneo ya Tanzania katika sekta ya afya.
Awali Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya
dawa Nchini MSD Laurean Rugambwa Bwanakunu,amesema magari ya bohari ya dawa MSD
sasa yatakuwa 213 kutoka magari 32 yaliyokuwepo ambapo magari hayo ya Land
Cruiser 104,Malori 77 ambayo kwa ujumla yamegarimu shilingi Bilioni 20.75.
Kwa upande wake Leindan Moris
mwakailishi wa Global Fund amesema wametoa msaada huo ili kuwezesha bohari ya
dawa MSD itoe huduma za jamii mara kwa mara katika vituo mbalimbali nchini.
Kwa mjibu wa waziri wa afya,maendeleo
ya jamii,jinsia,wazee na watoto Ummy Mwalimu kwa sasa Tanzania ina vituo vinavyotoa
huduma za afya vipatavyo 7284.
Habari zaidi ni WWW.P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments