MKUU WA SHULE AJINYONGA OFISINI KWAKE AKIMTAJA MKURUGENZI
MKUU
wa Shule ya Sekondari Kakonko wilayani Kakonko mkoani Kigoma,Peter Rubonya
amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kamba ofisini kwake mapema leo asubuhi.
Akielezea
tukio hilo,Mwalim wa zamu wa shule hiyo Isaac Japhet amesema yeye alifika
shuleni hapo saa 12:30 asubuhi ili kuwafundisha wanafunzi wa kidato cha nne
masomo ya ziada baada ya kufunga shule wiki iliyopita na baada ya kufika
aligundua kuwa hana chaki ambapo mkuu huyo wa shule alimpatia chaki mlinzi ili
awape wananfunzi.
Amesema
baada ya muda,Mratibu elimu kata pamoja na mmoja wa wazazi walifika ofisini
hapo wakiwa na shida na mkuu wa shule na baada ya kuelezwa yupo ndani ofisini
lakini baada ya kugonga mlango hawakuweza kujibiwa na ndipo wakaamua kufungua
mlango na kukuta mwili wa marehemu ukining’inia dalini.
Mwalim
Isaac amesema Mwalimu aliyejinyonga alikuwa akifundisha masomo ya Kemia na
Fizikia shuleni hapo hawakuwahi kusikia mgogoro wowote wa kifamilia au kijamii na
mkewe ambaye ni mkufunzi katika Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM),alifika nyumbani
kwake juzi akitokea Dodoma.
Kwa upande wa Mlinzi wa Shule hiyo Kajolo Kajabojabo amesema alikutana na Mkuu wa shule mapema asubuhi akiingia ofisini na kumuomba chaki ambazo alipewa na kuziwasilisha kwa walimu.
Kwa upande wa Mlinzi wa Shule hiyo Kajolo Kajabojabo amesema alikutana na Mkuu wa shule mapema asubuhi akiingia ofisini na kumuomba chaki ambazo alipewa na kuziwasilisha kwa walimu.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kigoma Martin Otieno amesema baada ya kupekuliwa kwa mwili wa
marehemu walikuta karatasi imeandikwa ujumbe kuwa Mkurugenzi wa halmashauri ya
Kakonko Lusubiro Mwakabibi asipodhibitiwa ataua wengi.
Habari zaidi ni WWW.P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments