ZAIDI YA SHILINGI MIL.9 ZATUMIKA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA SHULE KATAVI


Baadhi ya wajumbe wa kamati ya kulea baraza la watoto wenye ulemavu wilayani Mpanda(PICHA NA.Issack Gerald)
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya kulea baraza la watoto wenye ulemavu wilayani Mpanda(PICHA NA.Issack Gerald)
Mratibu wa Mradi wa elimu Jumuishi Mkoani Katavi Bw.Fortunatus Raphael amesema mradio huo unaosimamiwa na shirika la IFI,umetumia zaidi ya shilingi milioni 9 kukarabati miundombinu ya shule za msingi Nyerere,Shanwe na Kivukoni katika kipindi cha mwaka 2017/2018.
Raphael amebainisha hayo katika taarifa yake kwa wajumbe wa kamati ya kulea baraza la watoto wenye ulemavu wilayani Mpanda,kupitia kikao ambacho kimefanyika katika Ofisi za mradi huo mjini Mpanda.
Aidha Raphael amesema  Mradi umetoa msaada wa mafuta maalumu kwa ajili ya watu wenye ualbino 44 wakiwemo 25 wa Manispaa ya Mpanda na 19 Halmashauri ya Nsimbo pamoja na kugawa mavazi pia baiskeli kwa watu wenye ulemavu wa viungo.
Amesema muda wowote wanatarajia kuwahudumia watoto wenye ulemavu kwa mkoa wote wa Katavi has maeneo ya vijijini ambapo huduma imekuwa haifiki kwa kuwa mradio huo tangu mwaka 2012 umekuwa wilayani Mpanda ambapo kwa sasa huduma itafikishwa wilaya za Tanganyika na Mlele.
Kwa upande wao wajumbe wa mradi huo wakiwemo Bw.Serapion Rwegasira na Maria Nchagwa pamoja na mambo mengine,wamewashauri wazazi,walezi,walimu waliopatiwa mafunzo na serikali kwa pamoja kushirikiana kuwafichua watoto wenye ulemavu ili wapatiwe huduma mbalimbali muhimu hasa elimu.
Jumla ya walimu 26 wa shjule za Msingi Kivukoni na Shanwe wamepatiwa mafunzo ya namna ya kuwabaini wanafunzi wenye ulemavu pamoja na namna ya kufundisha wanafunzi walio katika mchanganyiko wa wanafunzi waliopo katika madarasa ya wenye ulemavu na wasio walemavu.
Aidha katika shule za Msingi Azimio,Kivukoni,Shanwe,Kashaulili na Mwangaza za Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda,jumla ya vilabu 174 vimeundwa kwa ajili ya kujadili masuala ya watoto na watu wenye ulemavu.
Makundi ya watoto wenye ulemavu wanaohudumiwa na mradi huo wapo katika makundi mbalimbali wakiwemo wenye ulemavu wa viungo,wasioona,viziwi na wenye ualbino.
Shirika la IFI linalosimamia mradi wa elimu Jumuishi lina washirika watatu ambao ni ICD,IAS na FPCT.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA