NYUMBA ILIYOTEKETEA KWA MOTO JUZI ,CHUMBA CHA MPANGAJI HASARA NI ZAIDI YA MILIONI MOJA NA LAKI TANO(1,500,000).
Na.Issack
Gerald Bathromeo-Mpanda
Imebainika kuwa janga la moto lililotokea juzi
katika Mtaa wa Mpadeco Kata ya Mkananyagio Manispaa ya Mpanda Mkoani
Katavi,umesababisha Bi.Grace Emmanuel Mkazi wa mtaa wa Mpadeco kata ya Makanyagio
kupata hasara ya Zaidi ya Shilingi Miloni moja na laki tano (1,500,000).
B.Grace
amesema Moto huo uliozuka mchana uliunguza Vitanda 2 vyenye thamani ya laki
tano na elfu sitini(560,000),Magodoro mawili 5 kwa 6 yenye thamani ya Shilingi
laki tatu(300,000),Maguni ya Mpunga 4 thamani yake zaidi ya Shilingi laki
2(200,000),Upotevu wa fedha taslimu Shilingi laki nne na nusu za mkopo
zilizopotea wakati wa uokozi na nguo ambazo tahamani yake haijafahamika.
Akizungumza
akiwa nyumbani kwake muda mfupi baada ya kutoka hospitali ya Wilaya ya
Mpanda,alikolazwa baada ya kuzimia kutokana mshtuko alioupata baada ya kupata
hasara hiyo,amesema kuwa hata hivyo hajatambua kiasi alichotumia kwa ajili ya
matibabu.
Hata hivyo amekwishafungua jarada Polisi ili ili kufanya uchunguzi wa tukio hilo ambalo lilitokea muda mfupi baada ya kubadili mifumo ya mita kutoka bili kwenda mfumo wa Luku ambapo kwa mjibu wa mama aliyepata hasara Meneja wa Tanesco alisema kuwa huenda kulitokea hitilafu ndani ya nyumba.
Hata hivyo amekwishafungua jarada Polisi ili ili kufanya uchunguzi wa tukio hilo ambalo lilitokea muda mfupi baada ya kubadili mifumo ya mita kutoka bili kwenda mfumo wa Luku ambapo kwa mjibu wa mama aliyepata hasara Meneja wa Tanesco alisema kuwa huenda kulitokea hitilafu ndani ya nyumba.
Bi.Grace amesema
anaishi na watoto wake 3,wadogo zake 6,mama yake 1 ambapo mume wake naye
alikatiwa rufaa ya kwenda kutibiwa Bugando mwanza baada ya kuugua na hivyo
kufanya idadi ya watu 10 wanaomtegemea yeye.
Kwa upande
wake mmiliki wa nyumba hiyo ambayo alisema kuwa haina bima,alisema kuwa
uchunguzi ufanyike ili haki itendeke ambapo mbali na kueleza kupata hasara ya
kusuka upya mfumo wa umeme katika nyumba hiyo itakayopatikana,pia amewaomba
wasamaria kujitokeza kumsaidia Bi.Grace kutokana na Hasara aliyoipata.
Hata hivyo
jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoani Katavi siku ya tukio walifika haraka mara
baada ya kupata taarifa kupitia simu waliyopigiwa na kufanikiwa kuzima moto huo
amabo kama wasingefika mpema nyumba nzima ingeungua na kusababisha hasara
zaidi.
Hata hivyo
serikali ya Kijiji kupitia kwa mwenyekiti wa serikali hiyo Bw.Bernad Nkana
amesema kuwa mpaka sasa amekwishafikisha taarifa rasmi kwa kamati za majanga
ngazi ya Tarafa na Wilaya ili kuangalia uwezekano wa kumsaidia Bi.Grace.
Mbali na
Majang aya Moto katika mtaa wa Mpadeco,pia mtaa huo umekuwa ukikumbw ana
majanga ya makazi ya watu kuezuliwa na mvua zinazoambatana na upepo ambapo
mwaka jana,miongoni mwa waliopatwa na janga la mvua zilizoambatana na upepo ni
Diwani wa kata ya Mpanda Hotel Mh.Liwali ambaye makazi yake yapo Mtaa wa
Mpadeco.
Majanga
mengine katika mtaa huo ni athari zitokanazo na mvua ambapo mawaka uliopita
kuliripotiwa vifo vya watoto vilivyotokana na kusombwa na maji.
BI.GRACE EMAMMNUEL ANAOMBA MSAADA KUPITIA 0757 61 61 60.
Kwa
maoni,ushauri au ukiwa na habari tutumie kupitia p5tanzania@gmail.com
Comments