MEI MOSI KITAIFA KUFANYIKA JIJINI ARUSHA
Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda,Biashara,Taasisi za Fedha,Huduma na Ushauri (Tuico),kimeanza maandalizi ya maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei mosi) mwaka 2018.
Akizungumza
katika semina ya kuelimisha na kubadilishana uzoefu iliyowashirikisha viongozi
wa matawi mbalimbali ya Tuico mwishoni mwa wiki,jijini Dar es salaam,Mwenyekiti
wa Tuico taifa,Sangeze alisema Shirikisho la Vyama vya Huru vya Wafanyakazi
nchini (Tucta),limekiteua chama chao kuwa mratibu wa shughuli zote za Mei mosi
kwa mwaka huu.
Alisema
baada ya kupewa fursa hiyo wanafanya vikao vya maandalizi na tayari wamepanga maadhimisho
hayo kwa mwaka huu.
Katibu
wa Tuico Boniface Nkakatisi,alisema maandalizi hayo yanaenda na mialiko ya
wageni watakaohudhuria ikiwamo wafanyakazi mbalimbali nchini,wanachama wa
Tuico,mabalozi kutoka nchi mbalimbali duniani.
Mwenyekiti
wa Tuico taifa,Paulo Sangeze alisema mgeni
rasmi katika maadhimisho hayo anatarajiwa kuwa Rais John Magufuli ambapo kitaifa yatafanyika mkoani
Arusha katika Uwanja wa mpira wa Sheikh Amri Abeid.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments