SERIKALI YATOA TAHADHARI UGONJWA HATARI WA DENGUE
Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu amewashauri wananchi kwenda vituo
vya tiba haraka mara baada ya kugundua kuwa wana dalili za ugonjwa wa dengue.
Mhe.Ummy Mwalimu |
Hayo ameyasema wakati alipotoa tamko
juu ya kuingia kwa ugonjwa wa dengue hapa nchini mara baada ya kufunga Mkutano
wa 65 wa Jumuiya ya Mawaziri wa Afya wa Nchi za Afrika Mashariki,Kati na Kusini
ECSA leo jijini Dar es salaam.
“Kuna dalili za Ugonjwa Dengue
zikiwemo homa ya ghafla,kuumwa kichwa hususan sehemu za macho, maumivu ya
viungo na uchovu.Dalili hizi huanza kujitokeza kati ya siku 3 hadi 14 tangu mtu
alipoambukizwa virusi vya homa ya Dengue hivyo.Wizara inashauri wananchi wasiwe
na hofu,bali mara tu wanapoona dalili za ugonjwa waende katika vituo vya
tiba"amesema Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy amesema wakati
mwingine dalili za ugonjwa huo zinaweza kufanana sana na dalili za malaria
hivyo wananchi wanaaswa kwamba,wakipata homa wahakikishe wanapima ili kugundua
kama wana vimelea vya malaria au Dengue,au sababu nyingine,ili hatua stahiki
zichukuliwe.
Waziri Ummy amesema ili kujikinga na
ugonjwa huo ni lazima Kuangamiza mazalio ya mbu kwa kufukia madimbwi ya maji
yaliyotuama au nyunyuzia dawa ya kuua viluwiluwi vya mbu kwenye madimbwi hayo
pamoja na Kujikinga na kuumwa na mbu kwa
kuvaa nguo ndefu muda wote hasa nyakati za mchana.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments