RAIS MAGUFULI AKUTANA NA MMILIKI WA TIGO,VIGOGO WA UJERMANI NA DENMARK NAO WAJITOKEZA IKULU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli
amekutana na Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Millicom International Services LLC
inayomiliki kampuni ya simu za mkononi ya Tigo Bw.Mauricio Ramos,Ikulu Jijini
Dar es Salaam.
Kwa mjibu wa taarifa ya mawasiliano ya ais Ikulu wamezungumza
kuhusu uwekezaji wa kampuni hiyo hapa nchini.
Kwa upande wake Bw.Mauricio Ramos amesema amekuja kumweleza
Mhe.Rais Magufuli kuhusu maendeleo ya kampuni hiyo ambayo imewekeza Dola za
Marekani zaidi ya Bilioni 1 (sawa na zaidi ya Shilingi Trilioni 2.23 za Tanzania)
katika miaka mitano iliyopita na imeajiri wafanyakazi zaidi ya 90,000 na
kuwafikishia mawasiliano Watanzania kwa takribani asilimia 90.
Aidha Bw.Mauricio Ramos amempongeza Mhe.Rais Magufuli kwa
jitihada zake za kupambana na rushwa na amebainisha kuwa juhudi hizo ni muhimu
katika kuharakisha maendeleo na kupunguza umasikini.
Naye Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame
Mbarawa Mnyaa amesema kampuni ya simu za mkononi ya Tigo ni ya pili kwa ukubwa
hapa nchini ikiwa na wateja Milioni 11.06 na imekuwa ikilipa vizuri kodi ambapo
mwaka 2017 ililipa kiasi cha Shilingi Bilioni 262.77.
Katika
hatua nyingine,Mhe.Rais
Magufuli amekutana na watendaji wakuu wa kampuni ya Ferrostaal kutoka nchini
Ujerumani na Denmark na Watendaji wakuu wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya
Fedha na Mipango na Wizara ya Nishati, ambapo wamejadili kuhusu mradi wa ujenzi
wa kiwanda cha kuzalisha mbolea Mkoani Lindi.
Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Waziri wa Viwanda, Biashara
na Uwekezaji Mhe.Charles Mwijage,Waziri wa Nishati Mhe.Dkt.Medard Kalemani na
Balozi wa Denmark hapa nchini Mhe.Einar Hebogard Jensen.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments