WAFANYABIASHARA KATAVI WAREJESHEWA FEDHA ZAO WALIZOTAPELIWA
Katibu wa jumuiya ya wafanyabiashara
Tanzania mkoani Katavi Bw.Robison Thompson Bumela amethibitisha fedha za
kurejeshwa kwa wafanyabiashara waliokuwa wakidai kutapeliwa na baadhi ya makambuni
yanayouza mashine za kielektronic (EFDs) hapa nchini.
Hatu hiyo meithibitisha leo Ofisini kwake wakati akizungumza na mwandishi wetu kuhusu hatima ya malalamiko ya wafanyabiasahara waliokuwa wakidai kutapeliwa fedha bila kupata mashine hizo.
Aidha Bw.Bumela amesema
wafanyabiashara wachache ambao hawajarejeshejewa pesa zao ni waliokuwa
wamelipia bila kupewa risiti na hivyo kuleta ugumu katika ushahidi ili kumbana
wakala aliyechuku fedha zao.
Hata hivyo katibu huyo amebainisha
kuwa miongoni mwa changamoto zilizopo katika matumizi ya mashine ya EFDs ni mashine
hizo kutotunza kumbukumbu kwa muda mrefu hali inayosababisha kumbukumbu kupotea
baada ya kufutika.
Kupitia mikutano mbalimbali ya
wafanyabiashara,Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga pamoja
na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Bi.Lilian Matinga walikuwa akiiagiza mamlaka ya ya
Mpato Tanzania TRA Mkoani Katavi kuhakikisha wafanyabiashara wanapata fedha au
mashine zao za EFDs kwa kuwa mawakala walikuwa wakifanya kazi hiyo kwa
kushirikiana na ofisi za TRA Mkoa.
Jumuiya hiyo iliyoanzishwa mwaka 2014
kwa sasa ina wafanyabisahara wanachama zaidi ya 150 ambapo zaidi ya wafanyabiasahara
10 walikuwa wametapeliwa na makampuni yanayojinasibu kuwa yanauza mashine za
EFDs miaka miwili iliyopita.
Kwa mjibu wa wafanyabiashara.mashine moja bei yake ni mpaka shilingi laki 8.
Kwa mjibu wa wafanyabiashara.mashine moja bei yake ni mpaka shilingi laki 8.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments