MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA MKURUGENZI MTENDAJI WA BILL GATES FOUNDATION
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Bill & Melinda Gates Foundation Bw.Rodger
Voorhies.
Makamu wa Rais amesema amezungumza
mambo mengi na Bw.Rodger hasa kuhusu masuala ya afya,uwezeshaji wanawake
kiuchumi,kuwatoa kwenye kilimo cha sasa na kuwaingiza kwenye kilimo biashara
lakini pia kuongeza thamani ya mazao na mambo ya masoko.
Makamu wa Rais alisema wamezungumza
namna ya kuwarasimisha wanawake wa vijijini na wanawake wakulima ikiwa pamoja
na uwezekano wa wanawake vijijini kuweza kupata mikopo.
Aidha Makamu wa Rais alizungumzia
suala zima la upatikanaji wa maji safi na salama hasa kwa wakazi wa jiji la Dar
es Salaam ambapo mara kwa mara kumekuwa na milipuko ya magojwa ya kipindu
pindu.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji
wa Taasisi ya Bill & Melinda Gates Foundation Bw.Rodger Voorhies alisema
wamekuja kwa Makamu wa Rais kuzungumza juu ya shughuli zinazofanywa na taasisi
hiyo hapa nchini hasa katika masuala ya Kilimo na Afya na Mkakati Mpya wa
Kuwawezesha Wanawake Kiuchumi.
Aidha wameipongeza Serikali ya
Tanzania kwa hatua kubwa ambayo wamepiga katika kuwajumuisha wanawake katika
masuala yanayohusu Fedha.
Katika hatua nyingine,Mkurugenzi huyo
ameahidi ushirikiano mkubwa kwa Serikali ya Tanzania katika kutekelezaji wa
miradi ya taasisi yao.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments