VYUO 163 TANZANIA VYAFUNGIWA UDAHILI
Baraza la Taifa la Elimu na Ufundi
(Nacte) limezuia vyuo 163 kudahili wanafunzi katika kozi mbalimbali ngazi ya
astashahada na shahada,baada ya kukutwa na upungufu ikiwako kutokuwa na walimu
wenye sifa.
Akizungumza leo,Machi 23 na waandishi
wa habari, Mkuu wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Nacte,DK Annastella Sigwejo
amesema walifanya uhakiki kwa vyuo 459,kati ya hivyo 296 ndivyo vimekidhi
vigezo vya kutoa elimu kwa kiwango kinachotakiwa.
"Kutokana na hali hiyo hivyo
ndivyo vinaruhusiwa kudahili wanafunzi kwa ajili ya kozi mbalimbali ngazi ya
astashahada na stashahada kwa muhula wa udahili wa Machi na Aprili mwaka huu.”
Amesema licha ya kwamba vyuo
vilivyosajiliwa viko 580 waliamua kujiridhisha kwa kuvifanyia uhakiki ambapo walifanikiwa
kuhakiki vyuo 459.
Nacte wanawashauri wanafunzi
kuhakikisha wanajiridhisha kuwa wanaomba kujiunga kwenye vyuo vilivyokidhi
vigezo.
Mkuu wa Kitengo cha Udahili, Twaha
Twaha amesema kuwa majina ya vyuo vilivyoruhusiwa kudahili yamewekwa kwenye
tovuti ya Nacte.
"Hivyo Nacte inashauri waombaji
wa udahili kujiridhisha kwa kuangalia hiyo orodha iwapo chuo anachokitaka
kinaruhusiwa kudahili,"amesema Twaha.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments