ACT-WAZALENDO KATAVI WATOA MAAZIMIO MIGOGORO YA ARDHI KATAVI
Chama cha ACT-Wazalendo mkoani Katavi kimeazimia kuishinikiza
serikali kuchukua hatua za utatuzi wa migogoro ya ardhi inayowakabili wananchi katika maeneo mbalimbali mkoani
Katavi.
Joseph Mona ambaye ni Katibu wa Chama cha ACT Wazalendo mkoani Katavi
akizungumza katika mkutano wa chama hicho amesema kikao hicho kilichofanyika
jana kililenga kufanya tahimini ya namna ambavyo serikali ya mkoa inavyoshughurikia
migogoro ya ardhi inayoendelea kufukuta.
Mona ametaja baadhi ya kero za wananchi zimetokana na serikali kuchukua
baadhi ya maeneo yaliyokuwa makazi ya wananchi kwa madai kuwa maeneo hayo yalikuwa katika hifadhi za misitu.
Aidha Mona ametaja baadhi ya maeneo yenye migogoro kuwa ni pamoja
na vijiji vya Litapunga,Luhafwe,Sitalike,Ugalla, Kanoge na Mpanda Ndogo.
Hivi karibuni Chama cha ACT-Wazalendo wakiwa wameambatana na
viongozi wa kijiji cha Sitalike pamoja na wananchi wa kijiji cha Sitalike
walifika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral Mstaafu Raphael
Muhuga kwa lengo la kuzungumza naye ili kutafuta hatima ya haki ya wananchi
walifukuzwa katika maeneo yao ilihali serikali ilikosea yenyewe kuwaondoa
wananchi kimakosa katika vijjiji ambavyo wananchi wanadai kuwa vilisajiliwa
tangu enzi za kuanzishwa kwa vijiji mwaka 1974.
Mwaka 2017 mwezi Agost mwaka jana,mamia ya wananchi katika vijiji
vya Mgorokani,kata ya Stalike na Kijiji cha Nsambwe Kata ya Kanoge waliondolewa
katika makazi yao kwa madai ya kukaidi maagizo ya serikali yaliyokuwa yakiwataka
kuhama katika vijiji hivyo kwa madai ya kuwa ni hifadhi za misitu.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments