WANANCHI NSIMBO WAOMBA KUBORESHEWA HUDUMA YA MAJI DIWANI AKATAA KUWEKA WAZI MIPANGO
Wananchi wa kijiji cha Mtakuja
kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi,wameiomba serikali
kushughulikia miundombinu ya huduma ya maji kijijini hapo ili wananchi waondokane
na tatizo la kutofanya shughuli za maendeleo kwa sababu ya kupoteza muda mrefu
wkifuatilia maji.
Wamesema serikali imekuwa ikisema
itaongeza mabomba ya maji ambapo mpaka sasa hakuna mipango inayotekelezwa kadri
siku zinavyosonga mbele licha ya viongozi mbalimbali wakiwemo Mbunge wa Nsimbo
na Diwani wa kata hiyo kutoa ahadi.
Mwenyekiti wa kijiji cha Mtakuja Daud
Peter Nyasio amekiri hali ya huduma ya maji katika kijiji hicho kuwa mbaya ambapom
amesema visima viwili vilivyopo havikidhi idadi ya wananchi zaidi ya elfu tatu
wa kijiji hicho wanaotakiwa kuapa maji.
Hata hivyo Reward Sichone ambaye
Diwani wa Kata ya Kapalala inayojumuisha vijiji vya Mtakuja,Songambele na
Kapalala ameiambia Mpanda Radio kuwa hana jambo lolote la kuzungumza na chombo
cha habari kuhusu suala la maji katika kata ya Kapalala kwani kila wanapoomba
pesa serikalini hazitolewi kama inavyotakiwa.
Kwa mjibu wa Mh.Sichone,kuna zaidi ya
shilingi milioni 400 zilizotengwa kwa ajili ya miradi ya maji katika kata ya
Kapalala zilizotakiwa kuletwa katika kata hiyo mpaka sasa hazijatolewa na hali
inayompatia wakati mgumu wa kuzungumza namna ya kutatua tatizo la maji.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments