TUNDU LISSU KUFANYIWA UPASUAJI WA GOTI
Mbunge
wa Singida Mashariki (CHADEMA),Tundu Lissu anatarajiwa kufanyiwa upasuaji mwingine
wa goti la kulia Machi 14,2018 katika Hospitali ya Chuo kikuu cha Leuven, Gasthuisberg
ili kumnusuru asipatikane na athari za mifupa kutojiunga kwa wakati.
Lissu
amebainisha hayo usiku wa kuamkia leo wakati alivyokuwa anawafahamisha umma juu
ya maendeleo ya afya yanavyoendelea huko alipo na kusema anaendelea vizuri na
matibabu na sasa anaweza kusimama kwa miguu yote miwili bila ya msaada wa
magongo ya kutembelea.
Mbunge
Tundu Lissu alishambuliwa na watu wasiojulikana tangu Septemba 7,2017 akiwa
mkoani Dodoma na kisha kupelekwa nchini Nairobi kwa matibabu na baada ya miezi
3 alipelekwa nchini Ubelgiji kwa hatua nyingine ya matibabu.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments