BARAZA LA WAKUNGA LATOA TAMKO


Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania limelaani na kutoa pole kwa Wauguzi kutokana na matukio yaliyofanywa na viongozi ikiwemo kuwekwa rumande na kupigwa katika mazingira yao ya kazi.
Taarifa kutoka katika baraza hilo,iliyotolewa na Lena  Mfalila imesema vitendo hivyo ni udhalilishaji na ni kinyume cha miongozo ya kisheria inayosimamia ushughulikiaji wa tuhuma za uvunjifu wa nidhamu na sheria wakati wa kazi.
Taarifa hyo imeongeza kuwa kumpiga mtumishi wakati akiwa kazini ni udhalilishaji na ni kinyume cha sheria. "Nidhamu ya Wauguzi na Wakunga inasimamiwa na sheria inayoitwa the Nursing and Midwifery Act, 2010 inayotoa mamlaka ya kuchukua hatua za kinidhamu kwa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania". 
Matukio hayo  ya udhalilishaji yanajumuisha tukio lililotokea Machi 7 mwaka huu katika Hospitali ya Wilaya ya Tandahimba ambapo Muuguzi Amina Luena Nicodemus aliwekwa ndani kwa amri ya Mkuu wa Wilaya kwa tuhuma za kuuza nguo za watoto akiwa kazini.  
Tukio lingine lililotokea tarehe Machi 8 mwaka huu katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu ambapo Muuguzi Hilda Ebunka alipigwa na Diwani akiwa kazini akitoa huduma. 
Viongozi wa kitaifa,ikiwa ni pamoja na Mhe.Waziri Mkuu,Mheshimiwa Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais TAMISEMI na Mheshimiwa Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto kwa nyakati mbalimbali wamekemea na kusisitiza mamlaka mbalimbali kuepuka kufanya vitendo vya udhalilishaji wa Wauguzi na Wakunga.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA