RAIS JOHN MAGUFULI ATOA AGIZO KWA WAZIRI WA VIWANDA,BIASHARA NA UWEKEZAJI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Dkt.John Magufuli amemwagiza Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji,Charles Mwijage kuhakikisha wamiliki wa viwanda vya ndani wanaajiri wazawa.
Ametoa agizo hilo leo Jumapili Machi 11,2018 wakati akizindua
kiwanda cha kufua vyuma cha Kahama Oil Mill mjini Kahama mkoani Shinyanga.
Rais amesema wananchi wazawa ndio waliompigia kura,hivyo
wapewe kipaumbele cha ajira katika viwanda hivyo huku akiwataka wamiliki wa
viwanda kuhakikisha wanatumia malighafi za ndani kutengeneza bidhaa badala ya
kuagiza kutoka nje ya nchi.
Kuhusu kiwanda cha chuma amesema malighafi inapatikana
nchini,hivyo iwapo mkurugenzi wa Kahama Oil Mill anahitaji yupo tayari
kumpa bure badala ya kuagiza nje.
Wakati huo huo amewataka Watanzania kununua bidhaa za ndani
ambapo amewataka wamiliki wa viwanda kutengeneza zenye ubora ili kuhimili
ushindani.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments