WAZIRI ATOA AGIZO KWA IGP DHIDI YA WATAKAOANDAMANA
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba amesema amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro kuwakamata watu wote ambao
wamepanga njama za kutaka kuwauwa watanzania katika maandamano ambayo
wameyapanga kuyafanya.
Mwigulu
ametoa hiyo wakati alipokuwa akitoa salamu zake kwa Rais Dkt. Magufuli aliyopo
Mkoani Singida katika ziara yake ya kikazi ambapo leo hii (Machi 11, 2018)
amezindua kiwanda cha Alizeti Mkoani humo na kusema kinachotafutwa katika
maandamano hayo ni namna ya watu wanatawanywa ili kusudi waje kulalamika kuwa
serikali ndio imeuwa watu wake.
Pamoja
na hayo,Mwigulu ameendelea kwa kusema "Mhe. Rais ndio maana unaona vinyago
vinyago vingi hivi kama hivi juzi alitokea kijana mdogo amesema ametekwa, eti
ametekwa na akapata muda wa kutafuta pafyumu na nguo za kubadilishia kule
atakapokuwa ametekwa.
Aidha,
Waziri Mwigulu amesema endapo ikatokea hata watu wakaandamana ndani ya nyumba
zao bado sheria itachukua mkondo wake dhidi ya watu hao.
Kwa
upande mwingine, Waziri Mwigulu amesema yeyote atakayethubutu kutaka kuharibu
taifa la Tanzania kwa kufanya vitendo vya uovu hawatoweza kumuacha salama.
Kwa
mjibu wa taarifa ambazo zimesambaa mtandaoni, maaandamano yanatarajia kufanyika
mpaka ikulu ya rais Aprili 26,2018.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments