MWENYEKITI WA BUNGE AKATISHA KUSOMWA MAONI YA UPINZANI
Msemaji
wa upinzani wa Wizara ya Katiba na Sheria,Ally Salehe amesusa kusoma maoni ya
upinzani ya Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali baada ya Mwenyekiti wa
Bunge,Andrew Chenge kukataa kusomwa kwa baadhi ya maneno yaliyomo katika maoni
hayo.
Salehe
alikuwa akisoma maoni hayo leo Januari 30 mwaka 2018 kwa niaba ya msemaji wa
Wizara ya Katiba na Sheria,Tundu Lissu aliyeko nchini Ubelgiji kwa matibabu
baada ya kushambuliwa kwa risasi Novemba 7 mwaka jana.
Maneno
yaliyozuiwa na Chenge kusomwa na upinzani ni kuhusu matukio ya uhalifu nchini,
likiwemo la kushambuliwa kwa Lissu.
Salehe
alianza kusoma maneno hayo lakini alipofika aya ya nne alikatizwa na Chenge
akimtaka asubiri, baadaye kumueleza kuwa lugha iliyotumika katika ukurasa kwa
kwanza na pili wa hotuba hiyo si ya kibunge.
Baada
ya kauli hiyo,Salehe amesema upinzani unaiamini na unaisimamia hotuba hiyo kwa
kuwa wabunge wote wanayo nakala yake,akaomba kuiwasilisha na kurejea kuketi.
Habari zaidi ni
P5TANZANIA LIMITED
Comments