RAILA ODINGA AJIAPISHA KUWA ‘RAIS WA WANANCHI WA KENYA’



Kiongozi  wa upinzani Raila Odinga (NASA) ameapishwa kuwa ‘Rais wa Wananchi’ wa Kenya licha ya kugomea uchaguzi mkuu wa marudio nchini humo.

Raila Odinga amefika  leo katika Uwanja wa Uhuru Park pamoja na viongozi wengine wakuu wa NASA akiwemo Moses Wetangula na Musalia Mudavadi na kujiapisha akishika Biblia.
Aidha, mgombea mwenza wake Kalonzo Musyoka wa Chama Cha Wiper hakuwepo wakati wa kuapishwa kutokana na kuhofia kukamatwa, ambapo Odinga amesema ataapishwa baadaye.
“Odinga amesema leo ni siku ya kihistoria kwa Kenya, hatua ya leo ni kuelekea kutoa udikteta na kuleta demokrasia Kenya, maelekezo mengine mtayapata baadae,” alisema Odinga baada ya kuapishwa. Awali Raila Odinga aliiambia kituo cha habari cha KTN kwamba shughuli hio ‘ si mapinduzi ya serikali’
Raila aligomea uchaguzi huo kwa sababu za kusema kuwa tume ya Uchaguzi nchini humo si ya Uhuru na haki. Uchaguzi huo wa marudio ulikuja baada ya Mahakama ikiongozwa na Jaji Maraga kutengua Uchaguzi wa awali uliofanyika 8 Agosti.
Katika uchaguzi huo wa Oktoba, Rais Kenyatta alitangazwa mshindi akiwa na kura 7.5 milioni ambazo ni sawa na asilimia 98 ya kura zilizokuwa zimepigwa.
Waliojitokeza kushiriki uchaguzi huo walikuwa 39% kati ya waliojiandikisha kupiga kura. Kenyatta aliapishwa kuwa Rais wa Kenya baada ya uchaguzi wa marudio mnamo tarehe 28/11/2017
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA