WANANCHI WATAKIWA KUTUMIA MAHAKAMA KUPATA HAKI
Wananchi
Mkoa wa Katavi wametakiwa kujenga tabia ya kuitumia mahakama kama Chombo cha
kupatia haki kama kichocheo cha kuimarisha dhana ya Utawala
bora hapa Nchini.
Katika picha katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Salehe Muhando akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Lilian Charles Matinga |
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Mheshimiwa
Salehe Muhando wakati wa uzinduzi wa wiki ya sheria ambayo imeanza
kuadhimishwa katika Viwanja vya mahakama ya wilaya Mpanda.
Kwa upande wake hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama mkoani Katavi,MH
Ommary Hassani Kingwele amesema dhima kubwa ya uwepo wa wiki ya elimu ya sheria
ni kuhakikisha kuwa wananchi wote wanapata uelewa wa sheria.
Madhimisho hayo ya sheria mwaka huu yaliyo na kauli mbiu ‘’matumizi ya tehama katika utoaji haki kwa wakati na kwa
kuzingatia maadili’’kilele chake kitakuwa Februari
moja mwaka huu na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa mkuu wa mkoa wa Katavi meja
jenerali mstaafu Rafael Muhuga.
Habari zaidini
P5TANZANIA LIMITED
Comments