NAIBU WAZIRI AWAKABIDHI SILAHA MADEREVA BODABODA MKOANI KATAVI TAYARI KUPAMBANA NA MIMBA ZA UTOTONI
Na.Issack Gerald
Naibu waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia Wazee na Watoto Dk.Faustine Ndugulile,amewataka waendesha pikipiki
Mkoani Katavi kushirikiana na serikali ili kutokomeza mimba za utotoni.
Dk.Ndugulile ametoa agizo hilo leo
wakati akitunuku vyeti kwa waendsha pikipiki 100 wa Manispaa ya Mpanda
waliohitimu mafunzo ya kidhibiti Mimba za utotoni huku akiwataka pia watendaji
wa wizara mpaka wilaya kote nchini kutatua shida zinazowakabili madereva hao.
Wakati huo huo Dk.Ndugulile
amekabidhi baiskeli tano kwa wasimamizi wa mashauri ya watoto Manispaa ya
Mpanda baiskeli ambazo zimetolewa na shirika la JSI la Marekani ili baiskeli
hizo zitumike kuwafikia watoto waishio katika mazingira hatarishi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
waendesha pikpiki Mkoani Katavi Mh.Asalile Mwakabafu amesema wao watahakikisha wanashiriki
kudhibiti mimba za utotoni huku akisisitiza serikali kusimamia watendaji wake
wasioshughulikia matatizo ya waendesha pikipiki Mkoani Katavi.
Kwa upande wake Chacha Maisol ambaye
ni Mkurugenzi wa Shirika la JSI la Marekani upande wa mikoa ya Nyanda za juu Kusini
amesema Wizara ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI iliwaelekeza
kutumia nguvu kubwa katika Halmshauri 84 kati ya hizo 83 zikiwa za Tanzania
bara na 1 upande wa Zanzibar.
Aidha Maisol amesema katika ukanda wa
Nyanda za juu kusini wanatoa huduma katika Halmashauri 23 za mikoa ya
Rukwa,Katavi,Songwe,Ruvuma,Njombe na Songwe ambapo jumla ya wasimamizi wa
mashauri 500 kutoka katika miko hiyo wamepatiwa mafunzo ili kuelimisha na
kudhibiti watoto waishio katika mazingira hatarishi.
Mkoa wa Katavi mpaka sasa unaongoza nafasi
ya kwanza kwa asilimia 45 kwa kuwa na watoto wenye mimba za utotoni kati ya
mikoa yote Tanzania.
Dk.Ndugulile aliyekuwa ameambatana na
watendaji wa wizara yake na wengine kutoka Tamisemi Ofisi ya Rais aliwasili
jana Mkoani Katavi na kufanya ziara katika Halmashauri za Mkoa wa Katavi.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments