UHABA WA VYUMBA VYA MADARSA MKOANI KIGOMA WANAFUNZI ZAIDI YA 2000 WAKOSA KUJIUNGA NA SEKONDARI.
Upungufu
wa vyumba vya madarasa wilayani Uvinza
Mkoani Kigoma imekuwa sababu ya zaidi ya wanafunzi 2000 kukosa nafasi ya kujiunga
na masomoa ya sekondari kwa mwaka 2018.
Kutokana
na hali hiyo,imewalazimu wakazi wa kijiji cha Nyanganga wilayani humo kuamua kuanza
ujenzi wa shule ya sekondari ili wanafunzi waliochaguliwa waanze masomo.
Wilaya
hiyo ina upungufu wa vyumba vya madaras 73 ambapo hata hivyo wanafunzi wengi wanalzamika
kusafiri umbali wa karibu masaa 3 kutoka nyumbani kufuata shule katika vijiji vya
jirani na wengine kulazimika kuhama nyumbani kuishi karibu na shule hizo.
Kama
sehemu ya kutafuta ufumbuzi wa changamoto hiyo, Naibu waziri wa Afya,Maendeleo ya
jamii,Jinsia,Wazee na watoto Dk.Fustine amechangia mifuko 20 ya saruji na kuwataka
wananchi kushirikiana katika miradi mbambali ya maendeleo yao.
Nao
Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Bw.MwanamvuaMlindo na Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza Weja Ngolo wametoa pamoja na kusema kuwa
wameweka mikakati ya kumalizia ujenzi wa vyumba vya madarasa vinavyojengwa na
kufikia katika hatua mbalimbali,wametoa wito kwa wananchi kuendelea
kushirikiana na serikli katika kutatua changamoto hiyo.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments